Ujumbe Muhimu Uliolengwa

1. Maradhi ya moyo yanazidi kuongezeka. Ndio kisababishi kikuu cha vifo miongoni mwa wanawake duniani kote.

2. Dalili za mshtuko wa moyo hazitambuliki katika zaidi ya 50% ya wanawake.

3+

Mbali na maumivu ya kifua, kuna uwezekano mkubwa zaidi ya wanawake kuwasilisha dalili 3 au zaidi, mbali na maumivu ya kifua.

Ukidhani kuwa mtu anapatwa na mshtuko wa moyo, tafuta msaada wa moyo mara moja.

DALILI ZA MSHTUKO WA MOYO ZINAZORIPOTIWA MARA NYINGI MIONGONI MWA WANAWAKE

  • Maumivu au usumbufu kwenye kifua
    (mfano shinikizo, kubanwa, au mchomo)
  • Maumivu kwenye taya, shingo, mkono, au mgongo
  • Kutokwa na jasho kupita kiasi
  • Kupumua kwa shida
  • Maumivu au usumbufu tumboni, au hisia za kichefuchefu au tatizo la umeng’enyaji wa chakula

DALILI ZINGINE ZINAZOAMBATANA AU ZINAZOHUSIANA NA MSHTUKO WA MOYO

  • Udhaifu au uchovu usio wa kawaida
  • Maumivu ya mgongo, bega au mkono wa kulia
  • Kukosa usingizi
  • Kizunguzungu au kisunzi
  • Mpigo wa moyo ulio wa kasi au usio wa kawaida

3. Aina ya maradhi ya moyo yanaweza kuwa tofauti kati ya wanawake na wanaume.

Baadhi ya wahudumu wa afya wanaweza kuwa hawajui tofauti ya aina za maradhi kati ya wanawake na wanaume.
  • Maradhi ya ateri za moyo
  • Maradhi ya valvu za moyo
  • Arrhythmia (mpigo wa moyo usio wa kawaida)
  • Kupasuka kwa ateri ya moyo (SCAD)
  • Ateri za moyo kuwa nyembamba
  • Kutofanya kazi kwa mishipa midogo (ugonjwa wa mishipa midogo)
  • Cardiomyopathy (ugonjwa wa misuli ya moyo) ya aina ya takotsubo (inayosababishwa na mfadhaiko)
  • Peripartum cardiomyopathy (moyo kudhoofika wakati wa au baada ya ujauzito)

4. Wanawake wanaweza kuwa katika hatari kubwa zaidi ya maradhi ya moyo kuliko wanaume.

Hali zifuatazo husababisha hatari kubwa zaidi ya maradhi ya moyo:

Matatizo fulani ya ujauzito
(mf. Kujifungua kabla ya muda, kisukari au shinikizo la damu wakati wa ujauzito, preeclampsia)

Kukoma hedhi mapema
(Wastani wa umri wa kukoma hedhi ni 50-52)

Ugonjwa wa uvimbe wa ovari

Magonjwa ya kimfumo ya uvimbe na kinga nafsia
(mfano. Rheumatoid arthritis, lupus)

Uvutaji sigara
(Wanawake wana hatari mara 3 zaidi ya wanaume kupata mshtuko wa moyo kutokana na uvutaji sigara)

Ugonjwa wa kisukari
(Kuna uwezekano mara 3 zaidi wanawake wanaoishi na kisukari kufa kutokana na ugonjwa wa moyo ikilinganishawa na wanaume)

5. Kuna mengi ambayo sote tunaweza kufanya ili kusaidia kupunguza hatari. Maradhi ya moyo yanaweza kuzuilika kwa kiasi kikubwa.

Fanya mazoezi ili kudumisha afya bora

Kula vyakula mbalimbali vyenye afya

Dhibiti mfadhaiko

Ishi bila tumbaku ya dukani na uvutaji wa mvuke

Punguza pombe

Pima afya mara kwa mara
(Pimwa kiwango cha sukari kwenye damu, shinikizo la damu na kolesteroli)

Ili uwatunze wengine, ni lazima kwanza ujitunze wewe mwenyewe.